Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema, licha ya Serikali kukusanya kodi kwa wananchi, bado kuna watumishi ambao si waaminifu wanaoendeleza vitendo vya rushwa na kuisababishia Serikali ikose mapato.
Mwigulu ameyasema hayo leo Juni 14, 2022 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka 2022-23.
“Wapo watumishi ambao bado wanaendelea na mchezo wa kuuza bidhaa kwa kutotoa risiti, wanasema ukihitaji risiti ni bei hii na usipohitaji risiti ni bei hii.
“Wanaofanya vitendo hivi waache mara moja kwani tukiwabaini si tu kwamba tutawahamisha kazi, tutawafukuza kabisa kazi,” alisema Mwigulu.