Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi wa chuo apigwa risasi na polisi, Mashuhuda waelezea tukio zima (Video)

Video Archive
Wed, 7 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Kiongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Meru nchini Kenya, Evans Njoroge ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi jana Februari 27, 2018 katika maanadamano chuoni hapo wakishinikiza chuo hicho kupunguza ada yao kwa kiasi cha shilingi 8,500 za Kenya ambazo ni sawa na Tsh 188,566 na kuboreshewa miundombinu chuoni hapo.

Evans Njoroge mwenye koti kwenye picha

Mashuhuda wa tukio hilo waliohojiwa na kituo cha runinga cha NTV wamesema kuwa wanafunzi wa chuo hicho baada ya vurugu walikimbia nje ya chuo na kwenda kujificha mashambani baada ya kuona gari la polisi.

Shuhuda mmoja ambaye mwanafunzi huyo ameuawa kwenye shamba lake la viazi vitamu, amesema kuwa maaskari baada ya kuwakosa chuoni walikuja uraiani walipomuuliza kama amewaona wanafunzi hao alikataa kuwajibu, lakini baadaye mtoto wake aliwaelekeza polisi wanafunzi hao walipojificha.

Baada ya dakika mbili mama huyo ambaye jina lake halijatajwa kwa sababu za kiusalama alisema alisikia mlio wa bunduki na alipotoka alimkuta askari anabadilisha mavazi yake na kubakia na nguo za kiraia.

Niliona wanafunzi wakikimbia nje ya geti la nyumba yangu wengine wakielekea mashambani, muda mfupi baadae nikaona polisi wakiingia getini kwangu wakiniulizia walikojificha sikuwajibu! hadi mtoto wangu alipowaambia, baadaye baada ya kumuona mwanafunzi huyo amejificha kwenye mti alimpiga risasi wakati alipotaka kumkimbia na akabadilisha nguo zake na kurudi kwenye gari,“amesema shuhuda kwenye mahojiano yake na Kituo cha NTV Kenya.

Kwa upande wa mashuhuda wengine wamesema kuwa polisi huyo aliyemuua mwanafunzi anafahamika ni Afisa wa jeshi la polisi la kituo cha Nchiru.

Taarifa kutoka kituo kingine kikubwa cha polisi cha Tigania, kupitia kwa msemaji mkuu wa kituo hicho, Kamanda Adamson Furaha amesema kuwa alisikia kuna maandamano na alituma polisi wa kuzuia maandano hayo.

Kwa upande wa uongozi chuoni hapo umesema kuwa umepata taarifa hizo na mwili wa mwanafunzi umepelekwa Hospitali kwa ajili ya majibu ya kitabibu. Tazama video aliyorekodiwa kabla kuuawa muda mfupi baadaye

Hata hivyo baada ya tukio hilo wanafunzi waliendelea kushinikiza makamu wa Rais wa chuo hicho, Japheth Magambo kujiuzulu nafasi yake kwani ndiye anayeharibu chuo hicho.

Baadhi ya Wakenya wakiwemo viongozi na wanaharakati wamelaani vikali tukio hilo la askari kujichukulia sheria mkononi, wengi wakisema kuwa ni tukio la kinyama.









Tayari jeshi la polisi nchini Kenya linafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, na Chuo hicho kilichotakiwa kufunguliwa leo Februari 28, 2018 kupitia mtandao wake kimatangaza kuahirisha hadi Machi 6, 2018.

 

 
Chanzo: bongo5.com