Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakyembe, Prof Kabudi walivyombananisha Jaji Warioba

Warioba Pc Data Jaji Warioba

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jaji mstaafu Joseph Warioba amesema kipindi alivyokuwa kiongozi wa Serikali aliwahi kupitia nyakati ngumu za kuulizwa maswali magumu na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) leo Septemba 19, 2024 Jjini Dar es Salaam, kilichowakutanisha wadau kujadili tathmini ya hali ya demokrasia nchini, Jaji Warioba amewataja Profesa Palamagamba Kabudi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk Serngondo Mvungi ambaye kwa sasa ni marehemu.

"Nilikutana na vijana wahadhiri wakali kwelikweli, wakaniweka kitimoto mmojawapo alikuwa Kabudi (Profesa Palamagamba), walikuwa wanauliza maswali magumu na sikuwachukia na baadaye wakaja kuwa marafiki zangu," amesema,

Amesema alikuwa anafanya hivyo kuiga utaratibu wa Rais Julius Nyerere ambaye wakati huo alikuwa akienda Ukumbi wa Nkurumah kuzungumza na wasomi kisha kuruhusu kuulizwa maswali.

Msingi wa kuyasema hayo ni uthubutu waliokuwa nao kwa wakati huo ambao ni tofauti na wa miaka ya sasa wa kusifia kila Jambo.

Kwa sasa Profesa Kabudi ni Waziri wa Sheria na Katiba akiwa pia ameshika nyadhifa mbalimbali wakati wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Dk John MagufulR (sasa marehemu) na ya sita chini ya Samia Suluhu Hassan,

Dk Mwakyembe ambaye baadaye alikuwa mbunge wa Kyela, naye alishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Naibu Waziri wa Ujenzi, Waziri wa Vchukuzi, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Sheria na Katiba na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live