Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musukuma awavaa wanaosema ukichomwa chanjo unageuka zombie (Video+)

Video Archive
Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma amesema Wananchi wasipuuze kuchanja Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID 19, na kuwataka Wananchi kuwapuuza Wanasiasa vigeugeu.

Aidha amezungumzia pia maneno yanayoendelea mitandaoni kuhusu chanjo hiyo ya Uviko- 19.

“Ugonjwa wa Covid upo na Serikali kama Serikali Mheshimiwa Rais  amefanya kazi yake kama Rais wa nchi ameleta dawa na wala hakuna mtu anaelazimishwa kuchoma ama kutumia dawa Covid 19 kwani ni hiari “- Msukuma

“Ila Watanzania nao wawe makini na Wanasiasa maana ni vigeugeu sana kuna watu ambao mwanzo walishadadia sana kuhusu mikusanyiko, mtu ambae haamini kama kuna Ugonjwa wa Corona tunapoteza ndugu zetu pale hospitali ya Bugando, atembelee tu ajionee inawezekana unashabikia lakini kufa utakufa pekee yako”- Musukuma

Chanzo: millardayo.com