Hospitali ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro imetoa taarifa ya ndugu mmoja atakayepewa kitambulisho ndiye atakayeruhusiwa kumuona mgonjwa aliyelazwa hospitalini hapo kwa lengo la kuepusha maambukizi ya magonjwa.
Afisa uhusiano wa Hospitali hiyo amesema utaratibu huo upo muda mrefu na watumishi wanawahudumia wagonjwa wapo wa kutosha kwani kuna watu ambao wanafika hospitalini hapo wakiwa hawana ndugu lakini wamekuwa wakitibiwa.
“Sisi tumekuwa tukipokea wagonjwa wa nchi zaidi ya elfu moja ndugu wa wagonjwa tumekuwa tukiwapokea zaidi ya elfu moja kwa wakati mmoja kwa hiyo unaona ni muingiliano mkubwa wa watu kwa wakati mmoja”-Gabriel Afisa uhusiano K.C.MC