Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Mengi asema nguvu za baba yao hazikwenda bure

56517 MTOTO+PIC

Thu, 9 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Abdiel Mengi, mtoto wa kiume wa aliyekuwa mwenyekiti mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi amesema nguvu na muda alioutoa baba yake kwa watu ambao huenda hata hakuwafahamu au havikuwa vitu visivyo na tija.

Ameyasema hayo leo Alhamisi, Mei 9, 2019 wakati akisoma wasifu wa baba yake katika ibada ya mazishi ya Mengi kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi mjini.

“Ni kama funzo kwetu kwa namna gani mtu unaweza kuwekeza katika mioyo ya watu, ni kitu kikubwa tulichokuwa tukikisikia ila tumekiona kwa mara ya kwanza na kimetugusa sana, ni lazima kuyaishi matendo yake,” amesema Abdiel.

Amesema watendaji wa kampuni za IPP, wamekuwa kama familia kwa sababu juhudi zao zilionekana katika kuhakikisha harakati alizokuwa akiendesha baba yao zinafanikiwa.

“Wengine vyeo tulikuwa tunavisikia tu ila hatuvijui, tulizowea kuwaita aunt (shangazi) tulizowea kuita uncle (mjomba) na wakati mwingine yeye mwenyewe tulimuita mwenyekiti kama wengine,” amesema.

Mbali na hilo, pia ametoa shukrani kwa vyombo vya ulinzi na usalama, ubalozi wa Tanzania katika nchi za Falme za Kiarabu na waombolezaji wote walioshiriki katika msiba huo.

“Ni dhahiri kwetu kuwa mapenzi yao yalimgusa mzee wetu, hatupo huko ila kile tulichokiona kwa kiasi fulani tunaamini ameguswa.”



Chanzo: mwananchi.co.tz