Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto alawitiwa na rafiki wa baba yake

Pingu 4 Mtoto alawitiwa na rafiki wa baba yake

Fri, 6 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama mmoja mkazi wa Kibaha Msangani anaiomba serikali iweze kumsaidia kupata haki ya mtoto wake wa kiume anayesoma darasa la tano baada ya kulawitiwa na rafiki wa baba yake ambaye kwa sasa ameachiwa huru baada ya kutekeleza tukio hilo.

Mama wa mtoto huyo anasema kuwa baada ya kutoa taarifa kituo cha polisi mtoto huyo alipimwa lakini hakuna ushirikiano anaoupata na mpaka leo kesi ya mtoto wake haijapelekwa mahakamani.

“Alimshika mtoto akamwambia ukipiga kelele ninakuua, twende huku… akampeleka porini huko kuna mkorosho mkubwa, ndiko alipomvua nguo na kumlawiti mwanangu akamwambia ukisema kwa mtu nitakuua, ole wako nikusikie, mtoto akaogopa kusema….

“Ilikuwa siku ya Jumapili usiku, ilipofika Jumatatu nikamuuliza unakufahamu sehemu zote akasema ndiyo, akaenda akanionesha sehemu zote, ya kwanza ni hapa, ya pili ni hapa na nyumbani kwake akanipeleka akasema ni hapa.

“Nikarudi nikapita kwa Mwenyekiti nikamwelezea akanipa barua ya kwenda polisi, nikaambiwa kumpeleka mtoto hospitali kumpima, muda ulikuwa umeenda na nanuli sina na niko peke yangu, nikaongea na yule afande akasema nenda ukabangaize upate nauli kesho tukutane kule kule Hospitali ya Tumbi usisumbuke tena kuja kituoni.

“Kesho yake tukampeleka mtoto akapimwa akabainika kweli ameharibika, tukarudi polisi kupata RB na process zingine zikakamilika. Yule mtu hakukamatwa mpaka saa 7 za usiku akaenda mume wangu na mgambo wakamkamata tukampeleka polisi, ndugu zake wakaja kumwekea dhamana akatoka, polisi wakasema nirudi nyumbani watanijulisha tarehe ya kesi.

“Mpaka sasa mtoto hajapata matibabu yoyote kutokana na ukosefu wa pesa n ahata kipimo cha magonjwa ya zinaa niliambiwa ni shilingi elfu tano lakini kwangu ni ngumu. Mpaka sasa mwanangu hajapata hata kidonge, ninachofanya ni kuchemsha maji ya vuguvugu na kumkanda, ninaomba serikali inisaidie” amesema mama wa mtoto huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live