Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto abakwa na kuuawa, DC "wahuni wote kamata" (+video)

Video Archive
Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Msichana wa miaka kumi mkazi wa Mtaa wa Rwazi kata ya Kahororo, Bukoba amekutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa ambapo taarifa za Madaktari zimeeleza kwamba alibakwa na kisha kuuwawa.

Revocatus John ambaye ni Baba yake Mzazi amesema Binti yake alikutwa na mkasa huo baada ya kutumwa kwenda dukani.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo amefika nyumbani alipozikwa Mtoto huyo kutoa pole sambamba na maagizo ya Serikali.

“Mazingira ya kifo chake ni Binadamu asilimia mia na ni uhalifu kwahiyo nimeliagiza Jeshi la Polisi liendelee kufuatilia nani alifanya hicho kitendo na katika hili Wahuni wote kamata tutajuana kulekule Polisi”———Deodatus Kinawilo

Chanzo: millardayo.com