Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpina amshukuru Samia kumuondoa Makamba Wizara ya Nishati

Samia Makamba Mpina Mpina amshukuru Samia kumuondoa Makamba Wizara ya Nishati

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuondoa aliyekuwa Waziri wa Nishati, January Makamba kweye wizara hiyo na Kumteua Dkt. Dotto Biteko kuwa waziri wa wizara hiyo.

Mpina amesema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hoja kuhusu bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Aprili 25, 2024 limepitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025 yenye jumla ya Shilingi 1,883,759,455,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na taasisi zake.

“Kuanzia Januari mwaka huu, hali ya umeme ieimarika, nipongeze kwa jitihada hizo na hasa Waziri (Biteko) ulipoingia tulianza kuona usimamizi kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere na sasa linakamilika. Tulikuona unakwenda ziara moja kwa moja kwenye maeneo yote ya uzalishaji umeme, ukafuta likizo za watumishi wako mpaka likizo zako ili kuhakikisha umeme unapatikana.

“Kulikuwa na sarakasi nyingi sana pale Tanesco, waliajiriwa watumishi sita bila usaili, bila ushindani na bila kutangazwa na haijulikani waliletwa kutoka wapi kwa ajili ya nini kwenye shirika muhimu kama lile, na hao ndiyo walileta katakata ya umeme iliyokuwa ikifanyika Tanesco hata EWURA haikuisimamia vizuri Tanesco kuhakikisha umeme unapatikana ipasavyo.

“Namshukuru Rais Samia Suluhu na kumpongeza kwa kumuondoa Waziri wa Nishati aliyekuwepo (January Makamba bila kumtaja jina), kumuondoa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, kuvunja bodi ya Tanesco na kukuteua wewe Dotto Mashaka Biteko kuwa Waziri wa Nishati ambaye umeonesha uadilifu na unyenyekevu mkubwa kwa wananchi kuwajibika kikamilifu, tunataka mawaziri wa aina yako.

“Sasa tunataka kazi moja tu, hakikisha unashusha bei za umeme kwa sababu bwawa limekamilika na wananchi wanataka umeme. Dhdibiti hitilafu zinazotoke, wananchi walipwe haraka hitilafu zinazpotokea na sababu nyingine zilizokuwa zikisababisha katakata ya umeme kutokea zidhibitiwe,” amesema Mpina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: