Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke na mme wazikwa kwenye kaburi moja Arusha "alipata ,mshtuko" (+video)

Video Archive
Fri, 18 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Simon Molele pamoja na mke wake Doris Mollel waliofariki kwa siku mbili tofauti wamezikwa pamoja kwenye makaburi ya familia katika kata ya Sekei mkoani Arusha baada ya mke kufariki kutokana na kupata mshtuko baada ya kupata taarifa za mme wake aliyekuwa akimuuguza kufariki.

Mdogo wa marehemu Johanes Molele amesema ndugu yake alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa UTI sugu na alifariki tarehe 14 mwezi wa sita na wakati wakiendelea na taratibu zamazishi walipata taarifa kwamba mke wake naye amefariki kutokana na mshtuko.

“Alionekana ana ugonjwa wa UTI na aliendelea kupata matibabu baada ya siku nne alifariki dunia na mke wake baada yakupata taarifa alipata mshtuko mkubwa na wamezikwa hapahapa”-Alfayo Molell mdogo wa marehemu

Chanzo: millardayo.com