Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkataba wa Bandari Bunge tumeshamaliza kazi yetu - Spika

SPIKA TULIA NEW Spika atoa maelekezo sakata la Bandarini

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson amewataka wabunge kuendelea kusikiliza maoni mbalimbali yanayotolewa na wananchi kuhusua suala la uwekezaji bandarini, lakini upande wao kuzungumza bungeni ulishapita na Bunge tayari lilimaliza kazi yake.

Hata hivyo amesema kwa vile kazi ya bunge ni kuishauri na kuisimamia serikali, inaweza kufanya hivyo pale serikali itakapoleta hoja zake bungeni kuhusu suala la mikataba itakayoingia.

Kutokana na hali hiyo, Dk Tulia amewataka wananchi wasihofu, kwani kazi ya Bunge ni kuishauri na kuisimamia serikali, hivyo ikiletwa bungeni hoja kuhusu mikataba wanayoingia, Bunge litafanyia kazi na kuishauri serikali.

“Ili tusiwe tunaenda mbele tunarejea nyuma kwa jambo mahususi linalohusu uwekezaji Bandarini, mawazo yaliyoendelea kutolewa na Wananchi baada ya Bunge kuwa limefanya maamuzi mwezi wa sita.

"Sisi kama Wabunge ni kazi yetu kuendelea kuwasikiliza Wananchi ili mawazo yao wakati utakapofika wa kuyatumia tuyatumie hayo kuendelea kuishauri Serikali na wakati utakapofika wa kuisimamia Serikali tutatumia mawazo hayo kuisimamaia Serikali"

"Bunge hili tulishamaliza kwa sehemu kazi yetu kazi itakayofuata baada ya hapo ni ya kuisimamia Serikali kwenye jambo ambalo Bunge limeshafanya maamuzi na kwa kuwa Bunge lilishafanya maamuzi tusije tukakuta katika Bunge letu hili tunarejea kutoa mawazo kwenye jambo ambalo tumeshalitolea maamuzi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: