Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkataba ujenzi daraja la jangwani kusainiwa

Jangwaniii Mkataba ujenzi daraja la jangwani kusainiwa

Tue, 3 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Daraja katika eneo la Jangwani jijini Dar es salaam ambapo mkataba unatarajiwa kuwa umesainiwa mwezi Septemba, 2024.

Bashungwa ameeleza hayo leo Septemba 02, jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Janeth Elias Mahawanga aliyehoji Lini Serikali itaanza rasmi ujenzi wa Daraja la Jangwani kuanzia Magomeni-Jangwani-Fire ili kuondoa adha wanayopata wananchi wakati wa mvua?

“Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) imepanga kujenga Daraja katika eneo la Jangwani lenye urefu wa mita 390 na kimo cha mita 15 ambapo hivi sasa taratibu za manunuzi zipo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba wake”, ameeleza Bashungwa.

Bashungwa ameeleza kuwa ujenzi wa Daraja la Jangwani utatumia fedha za mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maendelezo ya Bonde la Mto Msimbazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live