Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjane wa hayati rais wa Tanzania John Magufuli, Janet ni mgonjwa

E9fe6b852018a3a0 Mjane wa hayati rais wa Tanzania John Magufuli, Janet ni mgonjwa

Mon, 19 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kuugua kwa Janet Magufuli kulithibitishwa na mwanawe Joseph ambaye alifichua kuwa mama yake alipata mshtuko kufuatia kifo cha mume wake John Magufuli, Jumatano, Machi 17

- Kifo cha kiongozi huyo wa Tanzania kilitangazwa kufuatia wiki kadhaa za fununu baada ya kukosa kuonekana hadharani kwa wiki mbili

- Janeth ndiye aliteka moyo wa hayati huyo na kujaliwa watoto wanane pamoja

Mjane wa hayati rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, Janet Magufuli, anaugua

Kuugua kwa Janet kulithibitishwa na mwanawe Joseph ambaye alifichua kuwa mama yake alipata mshtuko kufuatia kifo cha mume wake John Magufuli, Jumatano, Machi 17.

Joseph, alizungumza Jumapili, Aprili 18, wakati alikuwa anatoa shukrani za familia hiyo kwa serikali ya Rais Samia Suluhu, viongozi wa kidini na maafisa wa usalama kwa wajibu wao kwenye mazishi ya Magufuli.

“Mama yangu (Mama Janeth) ana matatizo ya kiafya, alipata mshtuko kidogo baada ya Baba kufariki, anaendelea na matibabu hajaweza kuja lakini anawapenda sana Watanzania wote," alisema Joseph

Kifo cha kiongozi huyo wa Tanzania kilitangazwa kufuatia wiki kadhaa za fununu baada ya kukosa kuonekana hadharani kwa wiki mbili.

Kulingana na Rais Suluhu, Magufuli alianza kuugua na kupelekwa katika Hospitali ya Jakaya Kikwete Heart Institute Jumamosi, Machi 6.

Mnamo Jumapili, Machi 7, aliruhusiwa na madaktari kurejea nyumbani baada ya kukaguliwa na madaktari wa moyo.

TUKO.co.ke ilimuangazia Janeth Magufuli,62, mwanamke ambaye aliteka moyo wa kiongozi huyo na kujaliwa watoto wanane pamoja.

Wapenzi hao wawili walipenda kuweka mambo yao faraghani lakini wanaripotiwa kufanya harusi jijini Dar es Salaam.

Magufuli alikumbuaka namna alikosa suti na pete wakati wa harusi ake.

"Siku mimi nimefunga ndoa, sikuvaa koti, wala mke wangu hakuvaa shela. Tulienda kanisani Chuo Kikuu (UDSM)," alisema Magufuli.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke