Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili miwili kati ya mitano yaopolewa Bunda

Ziwa Uokoajiiiii Victoriaaaa.png Miili miwili kati ya mitano yaopolewa Bunda

Tue, 17 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miili miwili kati ya mitano iliyokuwa ikitafutwa baada ya mtumbwi kuzama katika Ziwa Victoria wilayani Bunda mkoani Mara imeopolewa leo Septemba 17, 2024.

Mtumbwi huo ulizama Septemba 15,2024 wakati ukiwa safarini kutoka Kijiji cha Mwiruruma kuelekea Kitongoji cha Bulomba kilichopo kwenye Kijiji cha Igundu wilayani Bunda.

Kuopolewa kwa miili hiyo miwili kunafanya idadi ya miili iliyoopolewa kufuatia ajali hiyo kufikia mitatu baada ya mwili mmoja kuopolewa muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Augustino Magere amesema miili iliyoopolewa imetambuliwa kuwa ni ya Nyanchugu Rasaro (39) na Machumu Machumu (32).

Amesema wanaendelea kutafuta miili mingine mitatu licha ya kuwepo kwa changamoto ya tope jingi na giza ndani ya maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live