Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ameliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha Shilingi 171.4 bilioni ili kuiwezesha wizara yake kutekeleza mipango mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Mabula amesema uidhinishaji wa bajeti hiyo yutasaidia kutekeleza mambo sita ya Wizara katika mwaka ujao wa fedha, na kwamba wataimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro ya ardhi na kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi.
Amesema, mambo mengine yanayotarajiwa kutekelezwa ni kuwekeza zaidi katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utunzaji wa, kumbukumbu, utoaji huduma na upatikanaji wa taarifa za ardhi pamoja na kuweka mazingira rafiki ya upatikanaji wa ardhi ya uwekezaji.
Wizara imepanga kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali yatokanayo na sekta ya ardhi ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia rahisi ya mawasiliano ya simu za mkononi; na kuimarisha mipaka ya kimataifa,” Waziri amelieleza Bunge.