Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa kwa kipindi hiki wameona watu kutekwa na kuteswa ikiwepo kupotea kwa wandishi wa habari wa kujitegemea wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Azory Gwanda.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mbowe alisema serikali haijatoa kauli yoyote iliyothabiti ya kwamba huyu mtu amekwenda wapi.
“Tumeona kwa kipindi hichi watu wanatekwa wanateswa wengine wanapotezwa waandishi wa habari nyie mtakuwa mashahidi Mwandishi mwenzenu bwana Azory amepotea sasa ni wiki karibia ya tatu katika mazigira sasa yakutatanisha akiwa chini ya vyombo vya dola, serikali haijatoa na kauli yoyote iliyothabiti ya kwamba huyu mtu amekwenda wapi taarifa ilivyo alimfuata mke shambani,” alisema Mbowe.
Azory anafanya kazi za uandishi wa habari Kibiti na Rufiji mkoani Pwani na ana siku 22 tangu atoweke kwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana Novemba 21.