Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfugale kuzikwa leo Iringa

F21e3a67aa339228e3db7a61b35725c7 Mfugale kuzikwa leo Iringa

Mon, 5 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWILI wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale (68) utazikwa leo kwenye makaburi ya familia Ifunda, mkoani Iringa.

Mfugale aliaga dunia Jumanne iliyopita katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Dar es Salaam, Rais Samia Suluhu Hassan aliwataka Watanzania wafanye kazi kwa bidii ili waache alama katika kila shughuli wanazofanya kama alivyofanya Mfugale.

“Ukipata umri acha alama, nawasihi Watanzania kuiga mfano wa Mfugale, huyu alikuwa baba wa barabara aliyetumikia taifa hili kwa hali na mali na kuacha alama iliyotukuka.”

“Kila mtu anapopata nafasi anapaswa kuacha alama, nawasihi Watanzania tujifunze kuacha alama katika kazi zetu tunazopata, naipa pole familia yake, mke, ndugu, wafanyakazi wenzake na watu wengine wote kwa pamoja,” alisema.

Rais Samia alimuelezea Mfugale kuwa alikuwa mtumishi kwa miaka 45, aliongoza Tanroads kwa miaka 12 na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa na kuongoza miradi ambayo haikuwa chini ya sekta yake.

Alisema hadi mauti yanamkuta, Mfugale alikuwa amekamilisha mchoro wa barabara za njia nne za mzunguko na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato, Dodoma.

Chanzo: www.habarileo.co.tz