Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara aliyevamiwa na kujeruhiwa Njombe afariki Dunia

Ndambo Njombeee Mfanyabiashara aliyevamiwa na kujeruhiwa Njombe afariki Dunia

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara maarufu katika mji wa Njombe, Godfrey Ndambo (45) aliyevamiwa na majambazi maeneo ya nyumbani kwake wakati akitokean kwenye biasharab zake na kupigwa na kitu kizito kichwani kilichosababisha majeraha, amefariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 22, 2024 amesema tukio hilo lilitokea Julai 20, 2024, saa 2:30 usiku katika eneo la Uzunguni, Kata ya Ramadhani, Halmashauri ya mji wa Njombe.

Banga amesema wahusika wa tukio hilo ambao idadi yao haijafahamika, walimpiga mfanyabiashara huyo na kutoweka na fedha zinazokadiriwa kuwa ni Sh47 milioni.

"Baada ya kujeruhiwa alitibiwa katika Hospitali ya Kibena na baadaye alihamishiwa mkoani Mbeya wakati matibabu yakiendelea akafariki dunia," amesema Banga.

Amesema jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi wa kina na baadaye watatoa taarifa ya watu watakaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.

Kamanda huyo amewataka wafanyabiashara mkoani Njombe kufunga kamera maeneo wanayoishi na ziwe wazi muda wote, kwani linapotokea tukio ni rahisi kwa polisi kuanza kufanya uchunguzi kupitia kamera hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live