Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta amezindua ujenzi wa barabara ya CCBRT kwa kiwango cha Lami, ambapo imekuwa mbovu kwa muda mrefu hali ambayo iliyopelekea kuleta shida kwa wakazi na madereva waliokuwa wakiitumia barabara hiyo.
Akizungumza Ijumaa hii mara baada ya kufanya uzinduzi huo, Meya Sitta amesema barabara hiyo ni miongoni mwa barabara muhimu katika Manispaa ya Kinondoni ,ambapo pia hutumika kwa wagonjwa wengi kuingia katika Hospitali ya CCBRT iliyopo Msasani eneo la Macho Jijini Dar es salaam.
Sitta ameeleza kuwa barabara hiyo imekuwa kero kubwa ,hivyo waandishi wa habari walikuwa wakimulika eneo hilo mara kwa mara ,na kubainisha kuwa tayari barabara hiyo imeshapatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake Meneja Mradi wa barabara hiyo Bw.Abdallah Yasin Msemo, amesema barabara hiyo itakamilika ifikapo tarehe 14-3-2018.
Ameongeza kuwa tatizo kubwa ambalo lilikuwa likiikumba barabara hiyo ni maji ambayo yalikuwa yakituama na kukosa eneo la kwenda,hivyo katika ujenzi huo utaambatana na mitaro itakayowekwa pembeni ya barabara hiyo ili kusaidia maji kupita panastahili.