Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amemuomba mganga mkuu wa manispaa hiyo,kuharakisha ukarabati wa Jengo lililonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kituo cha Afya cha Kigogo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhulia katika hafla ya kukabidhiwa hati ya Jengo, sitta amesema eneo hilo limenunuliwa na serikali kutoka katika kituo cha Dogodogo Center Street Children Trust(Caring for our Childen) kwa kiasi cha shilingi milioni 400.
Pia sitta amesema mahitaji katika sekta ya afya ni makubwa sana na hivyo serikali inajtahidi kupunguza bajeti kwenye vitu vingine na kuwekeza kwenye sekta ya afya ili wananchi waweze kupata huduma iliyo bora.
“Mahitaji ya wananchi wetu kwenye sekta ya afya bado ni makubwa sana ,lakini kigumu zaidi kwenye manispaa yetu ya Kinondoni tunaufinyu Wa ardhi wakuweza kujenga hospital kubwa Ila kwa kupitia kituo hichi kitaweza kuhudumia wananchi kutoka sehemu mbalimbali”Amesema Sitta.
Aidha amesema katika manispaa hiyo wanategemea kila mtaa uwe na Zahanati na kila Kata kuwe na kituo cha afya ili kufanikisha huduma iliyobora kwa wananchi,pia amesema wanategemea kujenga hospitali ya kisasa maeneo ya Magwepande ikiwa na lengo la kupunguza msongamano katika hospitali ya Mwananyamala,sambamba na kujenga hospitali itakayofanana na huduma za hospitali ya Apolo India ili kuweza kupunguza ongezeko LA wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
“Tumefanya jambo kubwa sana,mategemeo yetu kila Mtaa uwe na Zahanati na kila kata kuwe na Kituo cha Afya, ingawa tuna upungufu wa Zahanati 84, pamoja na vituo vya afya 18 na tumeanza mazungumzo ya kujenga hospitali za kisasa itakayosaidia kupunguza wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje na kuweza kutibiwa hapa hapa ” Amesema Sitta.