Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mengi asema dawa ya kutibu ulemavu ni upendo

47142 Pic+mengi

Mon, 18 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya PWDF, Reginald Mengi amesema dawa pekee ya kutibu ulemavu ni upendo.

Mengi ameyasema hayo leo Machi 17, 2019 wakati akikabidhi vitabu vilivyoandikwa kwa nukta nundu kwa ajili ya wasioona wakati tukio la utoaji wa tuzo za I CAN linaloendelea sasa katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hapa.

Vitabu hivyo vilivyotolewa (I Can I Must I Will) ni toleo la kitabu alichokiandika mwenyewe na kukizindua miezi kadhaa iliyopita, maudhui yake yakiwa ni hamasa kwa jamii kuhusu masuala ya ujasiriamali na uthubutu.

“Lazima tuwe na upendo, watu wenye ulemavu wana changamoto nyingi mfano za umasikini ni lazima tuwasaidie kwa vitendo na tujitahidi kuzungumzia uwezo wao pia,” amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa PWDF, Shimimana Ntuyabaliwe amependekeza kutolewa kwa  ruzuku kwa vyama vya watu wenye ulemavu, ili kuviwezesha kupanua wigo wa kazi zao kwa kufungua matawi katika ngazi za mikoa na wilaya na kata ili huduma ziweze kuwafikia walengwa kwa urahisi.

“Ruzuku hizi zitasaidia vyama hivi kuendesha shughuli zao katika misingi ya utawala bora ikiwa ni pamoja na kufanya uchaguzi kwa wakati hivyo kuondoa migogoro inayovikabili vyama,” amesema Ntuyabaliwe.

Aidha alimuomba ‘mgeni rasmi’ Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, vifaa visaidizi kama vile fimbo nyeupe, mafuta ya ngozi, viti mwendo, magongo yanayomlinda mtumiaji asiteleze kwa kuweka mipira maalum na vinginevyo kwa kuwa vimekuwa gharama.



Chanzo: mwananchi.co.tz