Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ateuliwa kuwania ubunge Mbarali

Bahati Ndingo Bahati Ndingo.

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati Kuu ya CCM imemteua, Bahati Ndingo kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika jimbo la Mbarali mkoani Mbeya.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi huo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Francis Mtega aliyefariki Julai Mosi kwa ajili ya pikipiki na gari jimboni humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa leo Agosti 17 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema uteuzi huo umefanywa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.

“Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Bahati Keneth Ndingo kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Mbarali, mkoani Mbeya,” imesema sehemu ya taarifa iliyotolewa na chama hicho.

Bahati ameteuliwa kufuatia ushindi alioupata katika kura za maoni katika jimbo hilo, akiongoza watia nia 25 waliogombea.

Mbali na jimbo la Mbarali, NEC ilitangaza uchaguzi mdogo wa udiwani kufanyika katika kata sita kutoka Halimshauri nne nchini.

Kata hizo ni pamoja na Nala (Halmashauli ya Jiji Dodoma), Mfaranyaki (Manispaa ya Songea), Mtyangimbole (Madaba), Old Moshi Magharibi (Moshi), Marangu Kitowo (Rombo).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: