Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ataka fidia majanga ya mto sokoni

Moto Manya Mbunge ataka fidia majanga ya mto sokoni

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa viti maalumu, Cecilia Pareso ameitaka Serikali ilieleze kwanini fidia hailipwi kwa wafanyabiashara ambao bidhaa zao huungua pindi moto unapozuka kwenye masoko husika.

Pareso ametoa hoja hiyo leo Jumanne Mei 10, 2022 bungeni alipokuwa akitaka kujua kauli ya Serikali juu ya matukio ya moto katika masoko yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Pareso ametaka kujua sababu za masoko kuendelea kuungua lakini wafanyabiashara husika wakiachwa waugulie maumivu wakati ni walipa kodi na masoko yanaungua kwa sababu ambazo si zao.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema si rahisi kujibu moja kwa moja kuwa watawalipa fidia kwani hakuna sheria inayosema hivyo ila wataendelea kuwapatia elimu.

Akijibu swali la msingi Sagini amesema hivi karibuni kumekuwa na matukio ya moto katika baadhi yamasoko nchini.

Amesema uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na vyombo vingine umebaini sababu mbalimbali za matukio hayo ni uunganishwaji holela wa mifumo ya umeme, kutokuzingatia tahadhari za moto kwa mama lishe na baba lishe na shughuli za uchomeleaji holela wa vyuma katika masoko.

“Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na vyanzo vya matukio hayo umefanyika ukaguzi wa kinga na tahadhari ya majanga ya moto sambamba na utoaji wa elimu na mafunzo ya matumizi ya vifaa vya awali vya kuzima moto katika masoko nchini,” amesema Sagini.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri, Serikali kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji inashirikiana na Halmashauri zote kuboresha miundombinu ya kuzima moto katika masoko na kuhakikisha ramani za masoko mapya zinakaguliwa na zinakidhi vigezo vinavyotakiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: