Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ataka ahadi za Rais kutekelezwa

Hamisi Tabasamu Pic Mbunge ataka ahadi za Rais kutekelezwa

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Sengerema (CCM), Hamis Tabasamu alalalamikia kutotekelezwa kwa ahadi za marais tena mbele ya viongozi wa juu wa Wizara ya Afya kuwa zitawatesa kwa wananchi.

Tabasamu ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 15, 2023 wakati akichangia katika makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya mwaka 2023/24.

Amesema aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli alipopita Busisi alitoa ahadi ya kujenga kituo cha afya mbele ya Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel lakini hadi leo halijatekelezwa.

“Hili jambo hadi sasa pengine linataka nikashindwe uchaguzi. Kuna laana nyingine zitakuwa zina nitafuna mimi kwasababu Molel (Dk Mollel) ulikuwepo ukija hapa (kuhitimisha bajeti) useme ni lini kituo cha Busisi kinakwenda kukamilika,”amesema.

Ametaka kuziheshimu ahadi hizo ahadi za marais wanapopita majimboni kwao kwasababu wanawaacha katika hali mbaya pindi vinapokuwa havipo kwenye bajeti.

“Mnakuja katika bajeti hivi vitu havipo, inakuwa hatari, naomba katika majumuisho yako useme kwanini hospitali (iliyojengwa jimboni kwake), hii haifunguliwi naomba majibu,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: