Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe kumburuza Mchungaji Msigwa mahakamani

Mbowe Kumburuza Mchungaji Msigwa Mahakamani.png Mbowe kumburuza Mchungaji Msigwa mahakamani

Fri, 6 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amevunja ukimya na kutangaza kusudio la kumfikisha mahakamani kutokana na kauli za mfululizo zinazotolewa dhidi yake na mbunge wa zamani wa Iringa Mjini kupitia Chadema, Mchungaji Peter Msigwa.

Mbowe ametangaza kusudio hilo kupitia barua ya notisi ya madai aliyomwandikia Mchungaji Msigwa kupitia jopo la mawakili watano – John Mally, Jonathana Mndeme, Hekima Mwasipu, Simon Mrutu na Dickson Matata.

Kwa notisi hiyo, amesema iwapo hatatekeleza masharti aliyompa ndani ya siku tano tangu kupata barua hiyo, atamfikisha mahakamani kutokana na kauli ambazo Mbowe anadai ni kashfa zenye lengo la kumshushia hadhi aliyoijenga kwa miaka mingi ndani na nchi na kimataifa.

Masharti ndani ya notisi hiyo ni kumtaka Mchungaji Msigwa kuchapisha taarifa katika kurasa za mbele za magazeti mawili (moja linalosambazwa kitaifa na lingine linalosambazwa kikanda), kwa namna na uzito sawa na kauli hizo, anazodai ni za uongo, ambazo amekuwa akizitoa dhidi yake katika vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali.

Katika taarifa atakazochapisha, Mbowe anamtaka Mchungaji Msigwa akiri na kuomba radhi kwa umma kwa kuchapisha habari za uongo kwa makusudi dhidi yake (akimtaja Mbowe kwa jina kamili).

Akizungumzia notisi ya mawakili wa Mbowe iliyoelekezwa kwake, Mchungaji Msigwa amekiri kupokea notisi hiyo na kuitia saini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live