Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda amesema, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe pamoja na viongozi wake, hawana uhungu na maisha ya vijana masikini ndio maana wanajilimbikizia mali.
Amesema, wanafanya kazi ya siasa si kwa manufaa ya wananchi bali manufaa yao binafsi,
"Wale ndugu zangu tunapaswa tuwapongeze na tuwapokee tukiwa tunafahamu wamechagua aina ya maisha na kazi yao inapatikana kutokana na ninyi kuhudhuria mikutano yao na sio kutatua matatizo yenu.
"Kama kweli Mbowe hoja yake ni ugumu wa maisha kwa nini asingeichukua ile milioni 150 akaenda kurudisha kwa vikundi vya vijana mamantilie na wauza genge kwamba chukueni huu mtaji nimepewa na Mama Samia?
"Nawapeni siri tu hata ile ofisi ya Chadema iliyopo pale Mikocheni mama kachangia.Kwa nini amechangia? Mama anasema tujenge demokrasia kwa sababu umekaa kwenye nyumba ya kupanga miaka mingi mno.
"Wale ndugu zangu wakija wasiwarubuni na Singida ni ngome ya Chama Cha Mapinduzi" alisema Makonda akiwa mkoani Singida.