Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe amtaka Rais Samia kuunda tume ya majaji kuchunguzwa waliotekwa

IMG 4340 Mbowe.jpeg Mbowe amtaka Rais Samia kuunda tume ya majaji kuchunguzwa waliotekwa

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan, kuunda tume ya kimahakama ya majaji, ili kuchunguza madai ya watu waliotekwa na kupotea nchini.

Mbowe ameyasema hayo leo Alhamisi Agosti 22, 2024, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mbowe amemuagiza Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika kumwandikia waraka maalum, Rais Samia juu ya suala hilo. “Rais chukua hatua, Watanzania wanaumia, wanauawa,”amesema na kuongeza kuwa kama hatopewa taarifa na wasaidizi wake, basi waraka huo umfikie moja kwa moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live