Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe: Maandamano ya Chadema yameruhusiwa na Jeshi la Polisi

Lema Mboweee.jpeg Mbowe: Maandamano ya Chadema yameruhusiwa na Jeshi la Polisi

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maandamano yasiyo na kikomo yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa ajili ya kupinga miswada ya marekebisho ya sheria za uchaguzi iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma, pamoja na kudai katiba mpya, yameruhusiwa na Jeshi la Polisi. 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, jana Jumatatu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amesema ruhusa ya maandamano hayo yaliyopangwa kuanza tarehe 24 Januari mwaka huu, imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro baada ya viongozi wa chama chake kuzungumza naye.

“Team yetu ya chama ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Bara, Benson Kigaila imekuwa na kikao na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Dar Es Salaam ACP Jumanne Muliro na timu yake kuhusiana na maandamano ya amani yanayopangwa na kuratibiwa na Chadema siku ya Jumatano, 24 Januari 2024,” ameandika Mbowe na kuongeza: “Makubaliano yamefikiwa kuwa maandamano yaendelee kama yalivyopangwa. Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa busara hii. Karibuni Watanzania wote, tuandamane kwa Amani. “

Chadema kiliitisha maandamano hayo yasiyo na kikomo hadi Serikali itapoondoa bungeni miswada hiyo iliyowasilishwa Novemba 2023, kwa ajili ya kuifanyia marekebisho kwa kujumuisha maoni na mapendekezo ya wadau yaliyoachwa, hususan la upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi pamoja na maamuzi ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhojiwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live