Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazungumzo ya Rais Samia na Waziri wa Marekani "tutapambana na corona" (+video)

Video Archive
Wed, 7 Jul 2021 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,  amezungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mhe. Antony Blinken.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken amempongeza Rais Samia kwa kushika hatamu ya uongozi nchini na kumhakikishia kuwa Serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Blinken amepongeza Rais Samia kwa hatua anazozichukua katika kukabiliana na ugonjwa  wa Corona nchini Tanzania na Marekani ipo tayari kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Aidha, Blinken amepongeza  jitihada za Rais Samia katika kuimarisha Demokrasia nchini ikiwa ni pamoja na azma yake ya kukutana na kushirikiana na Vyama vya Siasa  pamoja na kusimamia  Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Pia amepongeza uboreshaji wa mazingira ya ufanyaji biashara na kuahidi kuwa hali hiyo imeivutia Marekani kushawishi wawekazaji wake kuja kuwekeza nchini. 

Kwa upande wake, Rais Samia ameshukuru kwa pongezi na kuahidi kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya  Marekani kukuza uhusiano baina ya nchi hizi mbili katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa. 

Aidha, Rais Samia ametoa mwaliko kwa  Rais wa Marekani Joe Biden  kutembelea Tanzania ili kuzidi kuimarisha uhusino uliopo kati ya nchi hizi mbili.

KILICHOMSHANGAZA KIKWETE MPAKA AKAREKODI VIDEO “NI BAHATI KUONA SITAKI KUSIMULIWA”

Chanzo: millardayo.com