Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matapeli wa viwanja wanaswa Morogoro

Kamanda Wa Polisi Mkoa, Alex Mkama Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro - Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Alex Mkama

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wa matukio ya utapeli na udanganyifu ambapo watuhumiwa hao walikuwa wakiuza Viwanja ambavyo sio vyao.

Akizungumza na waandishi wa habari Julai 22 mwaka huu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro - Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Alex Mkama amesema katika Operesheni zilizofanywa kuanzia Julai 1 za kudhibiti hali ya usalama kwa kufanya misako na kusimamia mifumo ya ulinzi na usalama wamefanikiwa kuwakamata watu watatu ambao walikuwa wakijihusisha na uuzaji wa Viwanja ambavyo sio vyao.

Watuhumiwa walionaswa ni John Peter (50) mkulima mkazi wa Mkundi, Jibu Dotto (35) mkulima mkazi wa Mazimbu, Mwanaid Juma (43) mkulima mkazi wa kichangani.

Watuhumiwa hao walikamatwa Julai 17 mwaka huu katika manispaa ya Morogoro wakituhumiwa kujipatia zaidi ya Milioni 40 kwa kuwauzia wananchi Viwanja vya makazi katika maeneo ya watu wengine ambapo watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa wanaandaa mikataba ya uongo ili kuendelea kuuza Viwanja katika eneo la mkundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live