Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maswi ateuliwa tena Katibu Mkuu

Maswi Ateuliwa Tena Katibu Mkuu .png Maswi ateuliwa tena Katibu Mkuu

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Eliakim Maswi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Awali, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

Maswi aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anachukua nafasi ya Mary Makondo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.

Mary anachukua nafasi ya Rehema Madenge aliyestaafu.

Uteuzi huu umetangazwa jana Jumapili, Julai 21,2024 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live