Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapacha wawili wanaosoma chuo kikuu wafia kwa mganga - Video

Video Archive
Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana wawili ambao ni mapacha, wakazi wa Kiwalani, Dar es Salaam wamefariki dunia kwa pamoja huku chanzo cha vifo vyao kikidhaniwa kuwa walinywesha chenye sumu.

Vijana hao waliokuwa wakisoma shahada ya kwanza (Kulwa ama Alifu alikuwa akisoma Chuo cha IAA na Dotto ama Khalifa alikuwa akisoma Chuo cha CBE) na hivi karibuni wamemaliza mitihani yao yam hula.

Taarifa za awali zilizotolewa na kaka wa marehemu zinadai kuwa, wadogo zake walimuaga mama yao kuwa wanakwenda kusomewa dua kwani walikuwa wakihisi kukabwa na majinamizi wakiwa wamelala usiku.

“Ni kama machale yaliwacheza, walipofika kule Buza kwa huyo mama kuwasomea dua wakanitumia location na namba yake ya simu wakaniambia tumekuja kusomewa dua. Baadaye akanipigia Dotto kuniarifu kuwa hali zao sio nzuri.

“Nilifuata location mpaka nikafika walipo lakini hali niliyoikuta, Dotto alikuwa hajitambui, Kulwa naye hali ilikuwa mbaya lakini alikuwa na nafuu, tuliwachukua tukampeleka Hospitali ya Aga Khan walipowapima wakasema hawawezi kuwatibu tuwapeleke Hospitali ya Temeke.

“Baada ya kufika Temeke walipokelewa wakaanza kutibiwa, Dotto alifariki akabaki Kulwa, tukaanza kufanya dua madaktari wakatuondoa ili wafanye kazi yao, lakini baada ya muda naye aliaga dunia,” amesema kaka wa marehemu.

Aidha, mama aliyedaiwa kuwafanyia dua na kuwapa vitu vinavyodhaniwa kuwa ni sumu anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi Zaidi huku majibu ya sampuli kutoka kwenye miili ya marehemu zikipelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kuchunguzwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live