Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yamweka sokono Bruno

Bruno Fernandes Still Captain Man United yamweka sokono Bruno

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bilionea Sir Jim Ratcliffe na mabosi wengine wa ngazi ya juu Manchester United wanajiandaa kupokea ofa ya kumpiga bei Bruno Fernandes baada ya timu hiyo kutaka pesa na kupunguza bili ya mishahara kwenye kikosi.

Kumekuwa na mazungumzo kuhusu kiungo huyo wa Kireno, ambaye amekuwa kwenye kikosi cha Man United tangu Januari 2020, akihusishwa na mpango wa kuachana na maisha ya Old Trafford baada ya kucheza vizuri msimu uliopita.

Tajiri Ratcliffe na mabosi wenzake wanafahamu wazi Fernandes ni nahodha wa mifano kwenye kikosi hicho.

Hata hivyo, timu inahitaji pesa na kuna mpango wa kupunguza bili ya mishahara, hivyo hawatafunga milango ya kumpiga bei mchezaji huyo endapo kama italetwa ofa tamu mezani.

Wakala wa Fernandes, Miguel Pinho amekuwa kwenye majadiliano na timu nyingi, ikiwamo Bayern Munich.

Barcelona nao wanatajwa kuwa kwenye orodha ya timu zinazohitaji saini ya mkali huyo na huenda ikapiga hesabu za kumsajili kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi.

Staa huyo wa zamani wa Sporting Lisbon anahitaji timu hiyo impe uhakika wa kufanya vizuri na kupata mafanikio. Fernandes analipwa mshahara wa Pauni 220,000 kwa wiki, lakini anataka awe mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi kama Marcus Rashford na Jadon Sancho.

Rashford analipwa mshahara unaofikia Pauni 365,000 kwa wiki kabla ya kodi, huku Sancho na Casemiro ni mastaa wengine kwenye kikosi hicho wanaolipwa mkwanja unaoanzia Pauni 300,000 kwa wiki.

Fernandes anafahamu wazi kwamba mkataba wake ujao unapaswa kuwa mnono kwa sababu anaelekea kufikisha miaka 30, hivyo hata kiwango chake cha uwanjani kitakwenda kushuka.

Na sasa anataka kufahamu mwenendo wa klabu huku ikiwa bado haitambuliki kuhusu hatima ya kocha Erik ten Hag, kama ataendelea kubaki kwenye kikosi hicho au atafunguliwa milango ya kutokea baada ya timu kuboronga kwenye ligi msimu uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: