Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania yatahadharisha kuwepo kwa upepo mkali

Mamlaka Ya Hali Ya Hewa Tanzania Yatahadharisha Kuwepo Kwa Upepo Mkali.png Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania yatahadharisha kuwepo kwa upepo mkali

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: Bbc

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetahadharisha kuwepo kwa upepo mkali wa zaidi unaozidi kilomita 40 kwa saa.

TMA imesema upepo huo unatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya kusini mwa bahari ya hindi katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Maeneo mengine ya ukanda wa Pwani ya kaskazini mwa bahari ya hindi katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuahirishwa kwa baadhi ya shughuli za baharini na kuharibika kwa miundombinu ya bahari.

Chanzo: Bbc