Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama aliyesaidiwa na Mafuguli aibiwa bajaji

Video Archive
Thu, 23 Sep 2021 Chanzo: millardAyo

Nyangoma James ni Mlemavu ambaye Hayati Dkt. Magufuli alimchangia Mil 5 Ubungo Dar es salaam June,2020 na akachangisha Watu wengine hadi ikapatikana zaidi ya Tsh. Milion 8 ambayo Nyangoma alinunulia Bajaji na akawa Dereva yeye mwenyewe akiwa anafanyia biashara, lakini Jumamosi Wiki hii Bajaji yake imeibiwa kwenye nyumba aliyopanga Kibaha, Mkoani Pwani.

Licha ya kuwa na Watoto watatu ambao wawili anawasomesha kwa sasa, Nyangoma pia anaishi na Baba yake Mzazi ambaye amepooza miguu na Bajaji aliyoinunua kwa msaada wa Hayati Magufuli ndio iliyokuwa inamwezesha kuwahudumia Watoto na Baba yake, namba za kumchangia 0758311341 (imesajiliwa kwa jina la Joyce Songora).

"Namuomba Rais Samia Mimi Mwanamke mwenzake anisaidie, Viongozi wengine wote, Taasisi na Watanzania wote kwa ujumla wanisaidie nipate hata Bajaji nyingine maana kwa sasa naishi kwa kusaidiwa tu Majirani hata sina cha kuniingizia pesa"

Jitihada za kuwatafuta Polisi ili kujua ulipofikia upelelezi wa tukio hilo la Bajaji kuibiwa bado zinaendelea.

Chanzo: millardAyo