Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama afariki akisafirisha mwili wa mwanae

MAITI YAPOTEA Mama afariki akisafirisha mwili wa mwanae

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wa Familia moja Wakazi wa Babati Mkoani Manyara wamefariki dunia kwa matukio tofauti hii ni baada ya mmoja wa Familia hiyo Amina Hamis Mnyaruge (42) kufariki akiwa Jijini Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu na wakati Familia ikisafirisha mwili wake kwenda kuzika Babati, gari hilo likapata ajali na kuua Watu wawili akiwemo Mwakuni Said(66) ambaye ni Mama mzazi wa Amina Mnyaruge.

Msemaji wa Famili hiyo, Issa Mnyaruge amesema Wanafamilia hao wakiwa njiani kutoka Arusha kuelekea Babati gari lao lililokuwa limeubeba mwili wa marehemu liligongana na gari nyingine na kutokea ajali hiyo iliyosababisha kifo cha Mama Mzazi wa Amina pamoja na Baba Mdogo wa Amina aitwaye Said Mnyaruge (54) ambaye ni Shemeji wa Mama huyo na Ndugu wengine ambao ni majeruhi wapo Hospitali wakipatiwa matibabu.

Miili ya marehemu hao imewasili jana Mjini Babati Mkoani Manyara Kwa ajili ya shughuli za maziko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live