Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda awatangazia neema walemavu kwenye msiba wa Mengi

56160 MAKONDAPIC

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kuendelea kuwashika mkono walemavu wa mkoa huo kama ishara ya kumuenzi Reginald Mengi.

Makonda amesema kwa jinsi ambavyo Mengi amekuwa akijitoa kuwasaidia walemavu, ameona njia ya kumuenzi ni kuwasaidia katika mkoa wake.

Akizungumza wakati wa kuaga mwili wa Mengi aliyefariki Mei 2, 2019 mjini Dubai, Makonda amesema kwa kuwa kila mmoja ana namna ya kumuenzi Mengi yeye ameamua kujitolea kwa kuwasaidia walemavu.

“Nitafanya jambo jema nikiendelea kuwashika mkono walemavu, nafahamu wako wengi ndani ya mkoa huu lakini kwa kuwa nimeshaonja baraka za kuwahudumia nawahidi wa mkoa huu, hakika sitawaacha nitawahudumia.

“Namuomba Mungu anipe neema na unyenyekevu mkubwa niendelee kuwa sikio la wanyonge, maskini na watu wasiokuwa na thamani kwenye jamii lakini Mungu amewathaminisha kwa kuwapa uhai,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz