Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda amtembelea mama Magufuli

Makonda Kwa Mama Magu.jpeg Makonda amtembelea mama Magufuli

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Ziwa amefika kumsalimia Bibi Suzana Magufuli ambaye ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.

Itakumbukwa enzi za uhai wake wakati wa Kampeni Uchaguzi mwaka 2020, Hayati Magufuli aliwahi kuizungumzia hali ya afya ya Mama yake, September 09,2020 ambapo alinukuliwa akisema “Nakushukuru Mama Maria Nyerere kwa kuja kuniombea kura, una umri wa Mama yangu, wewe unatembea, Mama yangu yupo kitandani kwa zaidi ya miaka miwili anakula kwa kutumia mipira, siku tuliyokutana uliniambia Mama yako anaumwa kwa makusudi ya Mungu ili wengine tupone"

Baadaye October 10,2020 Hayati Magufuli akanukuliwa tena akisema "Kila mara namfikiria Mama yangu ambaye miaka miwili yupo kitandani hawezi kuongea anaumwa, ila alisimama kwa ajili ya Watoto wake, najua Wanawake wananyanyaswa kwenye mirathi n.k, ndio maana nimemchagua Mama Samia anisaidie

Chanzo: www.tanzaniaweb.live