Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makamba asimulia hekaheka alizopitia uteuzi bodi ya Tanesco

Makamba Na Mafuta Makamba asimulia hekaheka alizopitia uteuzi bodi ya Tanesco

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nishati, January Makamba amesimulia vikwazo na mapingamizi aliyoyapata wakati wa kupata wajumbe wa bodi ya Tanesco huku wengi wakimkosoa kuwatoa wajumbe hao katika sekta binafsi.

“Haikuwa rahisi kupata bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), baada ya uteuzi watu walisema unataka kulipeleka wapi shirika hili watu wamezoea wastaafu tu, kuna mzee mmoja namheshimu aliandika hadi Makala ya kukosoa,”amesema.

Makamba ameyasema hayo katika Kongamano la Jukwaa la Fikra kuhusu safari ya Shirika la Umeme (Tanesco) katika mabadiliko kuliangaza Taifa linalofanyika leo Jumatatu Julai 31, 2023 ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live