Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makamba: Kuunganisha gridi ya taifa na Malawi kutanufaisha nchi yetu

January Makamba Kuongoza Usalama Bomba La Mafuta Makamba: Kuunganisha gridi ya taifa na Malawi kutanufaisha nchi yetu

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali za Tanzania na Malawi zimeingia makubaliano ya kuzalisha umeme Mto Songwe, wa megawati 180; pamoja na ushirikiano katika ujenzi wa miundombinu itakayounganisha gridi za mataifa hayo.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini leo Agosti 1, 2023; Waziri wa Nishati, January Makamba amesema uunganishaji wa gridi hizo, ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme kuunganisha nchi za Kusini mwa Afrika na gridi ya Taifa.

“Mradi wa ujenzi wa miundombinu kati ya nchi zetu mbili yaani ‘interconnector’ ni sehemu ya mradi mkubwa wa kuwa na gridi moja Kusini mwa Afrika, na Tanzania mpaka sasa ina miradi kadhaa ya kuiunganisha nchi yetu na nchi nyingine,” amesema na kuongeza;

“Hivi sasa tumemaliza manunuzi ya kuunganisha gridi ya taifa na gridi ya Zambia, ambayo itaenda Kusini mwa Afrika, na wenzetu (Malawi), nao wameunganisha gridi yao na Msumbiji. Miradi hii itanufaisha nchi zetu kwani mahitaji ya umeme bado ni makubwa, makubaliano yetu ni sehemu ya mkakati kupata umeme wa uhakikai katika uzalishaji.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live