Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makamba: China inaongoza kwa ukubwa wa biashara kati yake na Tanzania

January Yusuf Makamba Makamba: China inaongoza kwa ukubwa wa biashara kati yake na Tanzania

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema mahusiano kati ya Tanzania na China yamekuwa na manufaa makubwa ikiwemo eneo la biashara na uwekezaji.

Hayo ameyabainisha jana Septemba 26, 2023 akiwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya sherehe ya kusherekea miaka 74 tangu kuanzishwa kwa Taifa la watu wa Jamuhuri ya China iliyofanyika katika ofisi za ubalozi huo.

Katika maelezo yake Waziri Makamba amesema sekta hiyo imekuwa ikikua kwa kasi na China imekuwa moja kati ya nchi inayoongoza kwa kuleta mitaji mingi nchini.

"China inaongoza kwa ukubwa wa biashara kati yake na Tanzania na imekuwa ikipanda katika sekta ya utalii, tunajivunia mahusiano yetu yaliyodumu kwa miaka 60 sasa na kadri miaka inavyoongezeka ushirikiano wetu umekuwa," amesema

Amesema hata Rais Samia Suluhu Hassan alipewa heshima ya kutembelea China Mwaka jana kufanya ziara ya kitaifa na katika safari hiyo viongozi wote waliweza kusisitiza namna ya kuwa karibu.

Awali, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Richard Kasesela amesema ndani ya kipindi hicho chama hicho kimepata manufaa makubwa kwenye kuwanoa viongozi wake mafunzo ya uongozi.

"Sisi na chama tuna timiza miaka 59 ya diplomasia kati ya Tanzania na China na tunajivunia viongozi wengi wamepata mafunzo ya uongozi kutoka kwao.

"Kwetu ni sherehe na tunatimiza miaka 59 tunajivunia viongozi wetu wengi wamepitia mafunzo ya uongozi na tumepewa na China tunajivunia," amesema

Kwa upande wake Balozi wa China, nchini Tanzania Chen Mingjian, amesema ushirikiano wa taifa hilo na Tanzania ni wakihistoria na bado wako mstari wa mbele kuunga mkono maendeleo.

"Kupitia sherehe kama hii bado tunaendelea kudumisha ukaribu wetu uliohenziwa na viongozi wa mataifa yetu mawili na kuendelea kuwa kitu kimoja, katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo " amesema

Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye na Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live