Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa awataka wataalam wa kilimo kutokaa ofisini

70498 Ofisi+n+pic

Fri, 9 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bariadi. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaagiza wataalam wa kilimo, mifugo na uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo, Jeshi la Kujenga Taifa na Magereza kwenda vijijini kwa wakulima kuwafundisha mbinu bora ya kilimo chenye tija.

Akitembelea bustani ya mbogamboga katika mabanda ya JKT katika viwanja vya maonesho ya Nyakabindi wikayani Bariadi leo Alhamisi Agosti 8, 2019, Waziri Mkuu pia ameagiza shughuli zinazofanyika katika bustani na mashamba ya taasisi hizo ziwe za kudumu kuwezesha wakulima kutembelea na kujifunza.

"Msisubiri hadi wakati wa maonesho ya Nanenane,  mashamba na shughuli hizi (za kilimo) ziwe za kudumu kipindi chote cha mwaka ili wakulima watembelee na kujifunza," ameagiza

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa Luteni Kanali Peter Lushika kuhusu shughuli zinazofanywa JKT katika maonesho hayo ya kitaifa.

Ili kutekeleza maelekezo hayo, Waziri Mkuu amezitaka JKT, Magereza na Wizara ya Kilimo kuandaa na kutekeleza programu ya pamoja kupitia halmashauri kufundisha wakulima kilimo chenye tija.

"Katika maeneo yenye vikundi vya wakulima kuanzia kumi na kuendelea hakikisheni mnachimba visima kuwezesha kilimo cha umwagiliaji," ameagiza Waziri Mkuu

Pia Soma

Kuhusu kilimo cha mbogamboga, kiongozi huyo ameagiza liwe moja ya ajenda muhimu akisema ni kati ya njia kuu za kuwezesha wakulima wenye maeneo madogo kulima kwa tija na kunufaika kupitia sekta ya kilimo.

"Bariadi na eneo kubwa la Mkoa wa Simiyu ni kame lakini ninyi (JKT) mmeweza kilima kwa sababu mmechimba visiwa. Wawezesheni wakulima siyo tu kujifunza kutoka kwenu, bali pia kumudu kilimo cha umwagiliaji kwa kuwachimbia visima.”

"Ili haya yote yafanyike na kufanikiwa nawataka Wataalam msikae kuwasubiri wakulima wawatembelee. Nendeni huko vijijini kwenye mashamba yao mkaone kilimo chao, muwashauri na kuwawezesha," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz