Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa avunja makundi Monduli

B3cafd9ae54f6ff9797005f429621a5b Majaliwa avunja makundi Monduli

Fri, 4 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza kuvunjwa makundi ya wanachama wa chama hicho waliowania ubunge katika jimbo Monduli mkoaniArusha.

Amewataka wanaCCM hao washirikiane kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo.

Amewaomba wakazi Monduli na Watanzania wote wamchague mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli ili aendeleze kazi ya kuwaletea maendeleo.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Monduli kwenye mkutano wa kampeni za CCM, kumuombea kura Magufuli na wagombea wa ubunge na udiwani.

"Kazi iliyonileta hapa ni kuwaomba kura wanaArusha na wanaMonduli, naomba kura zenu zote bila ya kujali itikadi za vyama vyenu, tumpigie kura Mheshimiwa Rais Magufuli na mgombea ubunge Fredrick Lowassa na wagombea wote wa udiwani kupitia CCM,"alisema Majaliwa.

Alisema, wananchi wanafahamu kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli, hivyo aliwaomba wamchague tena, kwa kuwa miradi mikubwa ya kimkakati aliyoitekeleza kwenye maeneo mbalimbali nchini, imegusa wananchi wengi.

Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, imeweka msisitizo kwa serikali kuleta mageuzi ya utalii, kilimo, mifugo na uvuvi ili kuwa na uhakika wa chakula na kujitegemea kwa chakula wakati wote na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi.

"Tutahakikisha uzalishaji unaongezeka katika sekta ya mifugo, utalii na uvuvi kwa ajili ya kuongeza tija katika kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuchochea maendeleo ya uchumi, hasa katika sekta za viwanda na huduma za jamii. Fugeni kisasa mpate faida na serikali ya CCM itaendelea kuwaunga mkono,"alisema Majaliwa.

Alisema, tayari vijana wengi wamenufaika kupitia sekta hizo, hivyo ni lazima serikali iendelee kuziboresha zaidi.

Chanzo: habarileo.co.tz