Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa atua Iringa, ataka ushirikiano

77173 Pic+majaliwa

Wed, 25 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema mahusiano kati ya Serikali na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa kidini, kimila ni muhimu yakaimarishwa.

Ameyasema hayo jana Jumanne, Septemba 24, 2019 wakati akipokea taarifa ya mkoa wa Iringa alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Iringa kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Waziri Mkuu alisema ni lazima mahusiano hayo yakadumishwa katika ngazi zote kwa sababu Serikali ipo kwa ajili ya wananchi wote na inawahudumia bila ya ubaguzi.

Aliwataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia maeneo mbalimbali nchini wahakikishe wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na uwajibikaji wao uwe na tija.

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa watendaji wahakikishe suala la ukusanyaji wa mapato linapewa kipaumbele katika maeneo yao.

“Ukusanyaji wa mapato ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kwa sababu miradi ya maendeleo kama ujenzi wa shule haiwezi kutekelezeka bila ya kukusanya mapato.”

Pia Soma

Advertisement
Awali, akisoma taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi alisema mkoa huo umepewa zaidi ya Sh7 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za wilaya.

Alisema fedha hizo zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa hospitali kwenye Manispaa ya Iringa asilimia 98, Halmashauri ya wilaya ya Iringa asilimia 90, Kilolo asilimia 99 na Mufindi asilimia 89.

Mkuu huyo wa mkoa alisema mbali na fedha hizo za ujenzi wa hospitali pia Serikali imetoa zaidi ya Sh3 bilioni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, kiongozi huyo alisema wanaendelea na maandalizi. Mkoa una vijiji 360, mitaa 222 na vitongoji 2,216

Chanzo: mwananchi.co.tz