Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa atangaza neema reli ya SGR

22df76e9d64b8c03ca36f2595420f70b Majaliwa atangaza neema reli ya SGR

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua kipande cha pili cha ujenzi wa reli ya kisasa kuanzia Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida ambao kwa sasa umefi kia asilimia 56.6 huku ujenzi wake ukitarajia kukami

lika Februari mwakani.

Pia amewahakikishia wananchi wote walioachia maeneo yao kupisha mradi huo kuwa wote watalipwa fidia zao kulingana na taarifa zao za uthamini.

Reli hiyo inajengwa na Kampuni ya Yapi Markezi na hadi Machi Mosi mwaka huu, mradi wote ulikuwa na wafanyakazi 8,014, ambao 6,472 sawa na asilimia 81 ni Watanzania na 1,542 sawa na asilimia 19 ni raia wa kigeni.

Majaliwa alianzia ukaguzi wa kipande cha Ihumwa hadi Igandu na kuoneshwa kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa reli hiyo huku akisisitiza kuwa kukamilika kwa mradi kutaongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kupunguza muda wa safari.

“ Mpaka sasa mradi umefikia asilimia 56.6, kiasi hii ni nzuri na inaleta matumaini kuwa utakamilika mwakani, hivyo wananchi tujiandae,” alisema.

Alisema serikali imejizatiti kuimarisha sekta ya usafirishaji kwa kusafirisha abiria na mizigo kwa lengo la kukuza biashara na kuinua uchumi .

“ Tumefanya mikakati ya kuimarisha sekta ya usafirishaji kuanzia usafiri wa anga ambapo kila mkoa lazima kuwe na kiwanja cha ndege, pia tumeimarisha mtandano wa barabara na kuimarisha usafiri wa reli, lengo ni kumrahisishia mwananchi na kwa kufanya hivyo tutainua uchumi wa nchi na wa wananchi wetu,” alisema.

Alisema utekelezaji wa miradi ya kimkakati imethibitisha kuwa vijana wa kitanzania wanaweza kuajirika tofauti na dhana iliyokuwa ikijengea huku akiwataka vijana walipoata fursa kuondoka na ujuzi waliojifunza kupitia kwa wataalamu wa mkandarasi huo.

Majaliwa alisema hakuna mwananchi ambaye amepisha mradi huo atapoteza haki zake.

Alitoa kauli hiyo wakati wa kujibu maombi yaliyotolewa na Mbunge wa Mvumi, Livingston Lusinde aliyesema kuna baadhi ya wananchi hawajalipwa fidia. Aliomba pia ijengwe shule iliyobomolewa kutokana na fidia ya Sh milioni 168 kutotosha kujenga shule nyingine.

Pia alishauri Sh bilioni 2.5 kati ya Sh blioni 5 ambazo mkandarasa anazipeleka halimashauri kuchangia miradi ya maendeleo zirudishwe serikalini kuchangia ujenzi wa reli hiyo.

“Hakuna mtanzania atakosa haki yake, niwahakikishie kuwa watalipwa wote kulingana na taarifa zilizopo kwenye uthamani wa fidia,” alisema.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kupunguza muda wa safari, mfano kutoka Dar es Salaam – Dodoma muda utakuwa saa tatu badala ya saa nane za sasa.

Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waliopata kazi katika mradi huo wafanye kazi kwa uaminifu na weledi wa hali ya juu ili kuudhihirishia ulimwengu kwamba Watanzania wanaajirika.

“Endeleeni kuchapakazi nyinyi ni mabalozi mtakaowawezesha wengine kupata ajira.

” Aliwataka Watanzania kuhakikishe wanaielewa vizuri shughuli wanazofanya katika mradi huo ili baadaye waweze kuisimamia wenyewe reli hii ikiwa ni pamoja na kufanya ukarabati.

“Tumieni ujenzi wa mradi huu kama sehemu ya kupata utaalamu.

” Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema ujenzi wa kipande cha pili cha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro hadi Makutupora umefikia asilimia 56.1 na unatarajiwa kukamilika Februari, mwakani.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kutashusha gharama za usafirishaji mizigo kati ya asilimia 30 mpaka 40 na kuifanya bandari ya Dar es salaam kuhimili ushindani.

Kipande cha kutoka Morogoro – Makutupora chenye urefu wa kilometa 422 kinajengwa na Kampuni ya Yapi Merkezi kutoka nchi ya Uturuki kwa gharama ya Sh trilioni 4.4.

“Reli hii itachochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati hususani nchi zisizopakana na Bahari, hivyo kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa.

Pia mradi huu utachochea uanzishwaji wa viwanda katika maeneo mengine ya nchi kwa kuwa utoa uhakika wa usafirishaji wa mali ghafi na bidhaa.” Kadogosa alisema hadi Machi Mosi mwaka huu, mradi huu ulikuwa na wafanyakazi 8,014, ambapo 6,472 sawa na asilimia 81 ni Watanzania na 1,542 sawa na asilimia 19 ni raia wa kigeni.

Alisema TRC imeendelea kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wataalamu wake mbalimbali, ambapo kwa sasa zaidi ya wataalamu 40 wanashiriki moja kwa moja kwenye ujenzi wa mradi wa SGR.

Chanzo: www.habarileo.co.tz