Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa atangaza kiama watafuna mali za ushirika

B25f196eb5fa57b076cea9e1ebc6927a Majaliwa atangaza kiama watafuna mali za ushirika

Sun, 4 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kulinda mali za ushirika itakapobaini zinataka kutafunwa na viongozi wachache wasio waadilifu.

Alisema hayo jana akihitimisha kilele cha Siku ya Ushirika Duniani iliyofanyika mkoani Tabora .

Majaliwa alisema watakuwa wakali kwa viongozi watakaofanya ubadhirifu ambao unarudisha nyuma maendeleo ya ushirika nchini.

Waziri Mkuu ambaye alisema wizi kwa mali za ushirika hilo ni janga kubwa, aliwataka viongozi wa ushirika kuwa wabunifu wa kuongeza mazao yao thamani kuongeza tija kwenye kilimo cha mazao mbalimbali yanayozalishwa .

Aliwataka viongozi wa mikoani na wilayani kufanya kazi za kutumikia wana ushirika ambao waliwachagua kwa ajili ya kuendeleza kilimo bila kufanya ubadhirifu .

Alipongeza uongozi wa vyama vikuu vya wakulima wa pamba wilaya Kahama na Chama cha Msingi Chato kwa kuwa na viwanda vya kuchakata pamba.

Alisema vyama hivyo ni vya vya mfano kwa kufanya vizuri na kuwa wabunifu kuongeza thamani ya pamba yao kwa kuichambua .

Awali, Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda alisema lengo la serikali kuingilia ushirika ni wananushirika wenyewe kushindwa kuusimamia na hivyo kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na sheria za ushirika nchini.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika, Theresia Chitumbi aliomba serikali kuongeza muda wa ukomo kwa viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika waweze kufanya vizuri kwenye utendaji wao wa kazi .

Chanzo: www.habarileo.co.tz