Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa ataka wanaopandishwa vyeo kuongezewa mishahara kwa wakati

88954 Majaaliwa+pic Majaliwa ataka wanaopandishwa vyeo kuongezewa mishahara kwa wakati

Wed, 18 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaagiza maofisa utumishi wote kuwapandishia mshahara watumishi wa umma wanaopandishwa vyeo ili kuiepusha serikali na madeni ya malimbikizo ya mishahara.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumanne Desemba 17, 2019 jijini Dodoma kwenye katika hotuba yake kwenye mkutano mkuu wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.

Amesema kumekuwa na uzembe mkubwa kwa maofisa utumishi nchini ambapo baadhi yao huchelewesha watumishi kupanda mishahara hata baada ya kupandishwa daraja na cheo hivyo husababisha watumishi wengi kuidai serikali malimbikizo ya mishahara yao.

"Nawaagiza wote wanaohusika hasa maofisa utumishi pindi wanapopata nyaraka muhimu za mtumishi kupandishwa cheo wawabadilishie na mshahara wake mara moja ili kupunguza madeni yasiyo ya lazima kwa Serikali," amesema Hasunga

"Madeni mengi ya watumishi wa umma serikalini yamesababishwa na uzembe wa baadhi ya watendaji ambao wanaona kabisa mtumishi amepandishwa cheo lakini hawataki kumbadilishia mshahara, nina uhakika kama watumishi watabadilishiwa mishahara yao kwa wakati madeni wanayoidai serikali yatapungua."

Amesema Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na vyama vya wafanyakazi nchini na itaendelea kushirikiana nao katika kuleta tija kwa mustakabali ya nchi yao.

Akisoma risala ya TALGWU Ofisa habari wa chama hicho, Shani Kibwasali amesema changamoto kubwa inayowakabili watumishi wa umma ni kucheleweshewa kuongezwa mishahara yao baada ya kupandishwa vyeo na kuiomba serikali kulitazama hilo kwa uzito unaotakiwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz