Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa ataja siri ya amani Tanzania

Cb3c03458315913ccd3b203eb21c060c …Ataja siri ya amani Tanzania

Mon, 7 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema siri ya Taifa la Tanzania kuendelea kuwa na amani na kimbilio la watu kutoka nchi ambazo zimepoteza amani ni kwa sababu ya uwepo wa dini.

Amewapongeza viongozi wa dini zote kwa kuendelea kuliombea Taifa.

Amesema kuanzia Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli inaamini dini ni mkombozi na msingi mkubwa wa amani, mshikamano na utulivu nchini.

Aliyasma hayo jana katika kongamano lililoandalia na kituo cha Radio Safina kuliombea Taifa na viongozi wake wakati wa kujiandaa kwa Uchaguzi Mkuu.

Kongamano hilo lilifanyika katika uwanja wa Magereza Kosongo, Arusha.

"Serikali itaendelea kushirikiana na dini zote na Rais Dk Magufuli anaamini kwamba dini ina mchango mkubwa katika kulifanya Taifa kuendelea kuwa ana amani. Nawashukuru viongozi wa dini nchini kwa kuliombea Taifa na kulifanya liepukane na vikwazo vingi ambavyo vingeleta athari."alisema.

Majaliwa aliwasihi viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla waendelee kushirikiana kuliombea Taifa na wamuombe Mwenyezi Mungu aiepushe Tanzania na majanga ili nchi iendelee kuwa na amani.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Kimanta aliwahakikishia wananchi kuwa mkoa upo salama na kwamba wajitokeze kwa wingi kushiriki katika kampeni na wasikubali kutishwa.

Chanzo: habarileo.co.tz