Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa apitishwa na Bunge kwa asilimia 100

937970746b415500b0ecacd9721a8250 Majaliwa apitishwa na Bunge kwa asilimia 100

Thu, 12 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Bunge la Tanzania, limempitisha Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kwa kupata kura zote 350 zilizopigwa na wabunge ambazo sawa na 100%.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma hii leo, Majaliwa amesema amepanga kupita maeneo mbalimbali ya nchi kujionea shughuli za maendeleo zinazosimamiwa na wabunge

“Tutapita katika majimbo yenu kukagua miradi mbalimbali pamoja na kupata fursa ya kukutana na wananchi ili kusikiliza kero zao na kutafuta namna bora ya kuzipatia utatuzi” amesema Majaliwa.

Amesema atahakikisha maendeleo yanapelekwa katika majimbo yote hata kwa yale ambayo yanaongozwa na wapinzani. Amemshukuru Rais Magufuli kwa uteuzi wake na kuhaidi ushirikiano kwa Bunge.

Chanzo: habarileo.co.tz