Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa afanya ziara Magomeni Kota

B12c2f8934d027a3f93bf1f371b139e6 Majaliwa afanya ziara Magomeni Kota

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye Mradi wa Magomeni Kota leo hata hivyo ameonyesha kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo.

Akizungumza leo amesema serikali inayoongozwa ipo makini na itaendelea kuwatumikia watanzania, na rais anasisitiza watanzania kuchapa kazi.

“Rais Samia anataka nchi hii iwe na amani na utulivu, tupendane, nchi ipo usalama, siri ya kuwepo maendeleo ni utulivu na amani, kama watu wake tutazungumza lugha moja tutafanikiwa sana.” amesema Majaliwa na kuongeza

“Watanzania tumeamua na tumejifunza tukiamua kusimamia kazi tunaweza kusonga mbele sio kuingiza vitu ambavyo tunapoteza muda, tutumie muda mwingi kujiletea maendeleo kuliko kutumia muda mwingi kujadili mambo yasiyofaa.” amesema

Akizungumzia mradi wa Magomeni Kota Majaliwa alisema anajua kuna changamoto nyingi za wafanyakazi na kuwatia moyo kuwa waendelee kuchapa kazi na kwamba serikali inatafutia ufumbuzi wa changamoto hizo.

“Najua kuna changamoto katika ujenzi huu lakini tunazitafutia ufumbuzi, hata sisi serikali kuna changamoto chungu nzima lakini tunafanya kazi, nawapongeza kwa kazi nzuri, licha ya changamoto mlizo nazo.

“Naamini wote mlishiriki kuchimba msingi, sina mashaka nanyi ubora huu umlionyesha itasaidia kupata kazi sehemu nyingine na nyingine, hakuna uwizi wa nondo kuna watu walikuwa wanaiba nondo?,…hakuna… kuna walioiba saruji, nyaya, misumari…. jipigieni makofi.” Majaliwa akiongea na wajenzi

Amesema “Jana nilikuwa Kibaha kuna Kampuni ya kuunda magari, imeajiri watu zaidi ya 100 sifa niliyopata watanzania sasa wafanyakazi ni waaminifu, hii inaleta taswira nzuri kwa nchi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz